Madaktari Bingwa katika Taasisi ya Mifupa ya Moi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbil(kulia) wakimpa Rais Jakaya Kikwete(shoto aliyevaa mavazi maalum) maelezo ya mgonjwa aliyejeruhiwa vibaya na moja ya mabomu yaliyolipuka katika ajali iliyotokea katika ghala la kuhifadhia dhana za kivita katika kambi ya jeshi la Wananchi wa Tanzania huko Mbagala, jijinji Dar es Salaam.Mgonjwa huyo amepoteza mguu wa kulia na amepoteza damu nyingi na napumua kwa kutumia mashine maalum (Life Supporting machine )
Rais Jakaya Kikwete akimpa pole mtoto Mariam Isihaka(8)aliyelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Temeke baada ya kuathirika kwa mshtuko kutokana na ajali iliyotokea katika ghala la kuhifadhi silaha katika kambi ya jeshi huko Mbagala jijini Dar jana mchana.Pembeni aliyeketi na Mtoto Miriam ni mama yake Husna Selemani mkazi wa Mtoni Mtongani, jijini Dar es Salaam
Comments