Thursday, November 15, 2007

MSHINDI WA BIG BROTHER HOUSE II, RICHARD BUZENHOUT AWASILI NCHINI



Mshindi wa Big Brother II Africa Richard akiwa katika kikao cha waandishi wa habari kilichofanyika katika hoteli ya Holiday Inn iliyopo maeneo ya Posta Jijini Dar es Salaam leo, kulia ni Meneja wa Multichoice hapa nchini (Lucy Kihwele) na kushoto ni mmoja wa maafisa wa Multi choice Baraka Shelukindo.


Baba mzazi wa Richard Bezuidenhout naye alikuwepo katika uwanja wa Ndege wa Jk Nyerere Jijini Dar es Salaam wakati wakimpokea mwanaye baada ya kushinda Big Brother Africa II.




Ndugu wa Richard,Louis naye alikuwa ni miongoni mwa Watanzania waliofurika kumpokea Mshindi huyo.



Ama kweli Richard ameleta mambo Mabaunsa , familia baba, kaka na dada zake , wabongo kibao walijaaa uwanjani hapo kuhakikisha usalama wa kutosha unapatikana na baadaye leo kazungumza na vyombo vya habari. Picha za Richard Bukos wa Global Publisherz na Mpoki Bukuku.

No comments:

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AMWAKILISHA WAZIRI WA FEDHA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI – ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde, amemwakilisha Waziri wa Fedha katika ufunguzi wa Kongamano la 16 la Mwaka la Wa...