Richard, ambaye alitambulika kwa uhalisia na mvuto wake ndani ya jumba la Big Brother, sasa anakutana na viongozi wa habari – akiwamo Yahya Charahani, Theophil Makunga na Sam Sollei – katika muktadha wa kuthamini ushindi wake si tu kama burudani, bali kama sauti mpya katika kizazi cha mawasiliano.
Tukio hili linazua tafakuri: Je, vyombo vyetu vya habari vina nafasi gani katika kuongoza simulizi za mafanikio ya vijana wa Kiafrika? Na je, umaarufu wa runinga unapotua kwenye dawati la habari, tunapata fursa ya kuibua zaidi vipaji vya ndani vinavyoweza kuchochea mijadala ya kijamii na maendeleo?
Kwa vyovyote, hii ni ishara ya kwamba mainstream media na majukwaa ya burudani vinaweza kushirikiana kuandika sura mpya ya Afrika ya sasa. Picha kwa hisani ya mdau Erick Kalunga.

2 comments:
Mh charahani salama mkubwa.?
hongera kwa kuliendeleza libeneke
kwa ujuzi wa hali ya juuu.. leo nimepita hapa kwako nakuchota mavumba kama kawaida..
kaza buti mkuu, tupo pamoja..
Admin
www.Haki-hakingowi.blogspot.com
sawa kaka hakuna mashaka tuko pamoja tunasonga mbele
Post a Comment