Waziri Mkuu wa Canada nomaaa

Hebu cheki hizi taarifa huyu jamaa Waziri Mkuu wa Canada aliyekuwapo jana hapa nchini kumbe ana soo, hivi karibuni
alipokuwapo huko Santiago, Chile alilazimika kuingilia mlango wa nyuma wa ofisi za kampuni ya Barrick Gold kukwepa kuzomewa.

Ilimbidi achelewe saa mbili huku akiwa chini ya ulinzi mkali uliojumuisha maboard guard, polisi na vikosi malumu, Stephen Harper (Waziri Mkuu wa Canada) aliwasili katika ofisi za Barrick Gold na akaingia kupitia mlango wa nyuma majira ya mchana akikwepa umati wa wananchi waliokuwa wakiandamana tangu saa mbili asubuhi.

Harper, anadhaniwa kufanya madudu kibao katika ziara yake hiyo ambayo amelazimika kuingia bongo akazungumza mawili matatu, lakini kwa baadhi ya madudu yake hebu mcheki hapa THE DOMINION NEWSPAPER eeee bwana noma kweli.

Comments