Monday, January 27, 2014

Waziri Mkuu Mizengo Pinda afanya ziara Mtwara atembelea maeneo mbalimbali

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akitembelea maeneo mbalimbali kinapojengwa kiwanda cha kuchakata gesi asili eneo la Madimba mkoani Mtwara wakati wa ziara yake mkoani Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa huo Kapteni mstaafu Joseph Simbakalia, kulia ni Mhandisi wa mradi wa kiwanda cha kuchakata gesi asili  Sultan Pwaga
 Meneja Mkuu Ujenzi kiwanda cha Dangote Tanzania Bhupendra Sharma akimwonesha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda moja ya mashimo ambapo itafungwa mitambo ya kiwanda cha kutegeneza saruji eneo la Msijute mkoani Mtwara.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akikagua baadhi ya vifaa ambavyo tayari vimeshafika eneo la Msijute mkoani Mtwara kinapojengwa kiwanda cha saruji cha Dangote Tanzania
 Mhandisi wa mradi wa kiwanda cha kuchakata gesi asili kilichopo katika eneo la Madimba kinachosimamiwa na Shirika la Maendeleo na Petroli Tanzania (TPDC) Sultan Pwaga akitoa maelekezo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda na Mke wake Mama Tunu Pinda wakimjulia hali moja ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mstafa J.Sabodo Chistopher Ngalapa (miaka 16 kidato cha pili) aliyelazwa katika Hospitali ya mkoa wa Mtwara Lugora baada ya kupata ajali tarehe Januari 22, 2014.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya sekondari Mstafa J.Sabodo wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipowatembelea shuleni humo kuwapa pole kwa msimba wa wanafunzi sita baada ya kugongwa na gari wati wa mchakamchaka karibu na eneo la shulke yao.Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO Mtwara

No comments: