Wednesday, January 29, 2014

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 37 YAPAMBA MOTO


Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Luteni Mstaafu Maganga Sengelema akifafanua jambo mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ikiwa sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambayo kitaifa mwaka huu inafanyika mkoani Mbeya.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Maganga Sengelema akimuonyesha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye sehemu ya kuweka jukwaa la waandishi wa habari kwenye uwanja wa Sokoine ambapo sherehe za miaka 37 ya CCM zitasheherekewa kitaifa.  
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa maandalizi ya awali katika uwanja wa Sokoine ambao unategemewa kufanyika kwa sherehe za mika 37 ya CCM tarehe 2 mwezi wa februari mwaka huu,mgeni wa heshima anategemewa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.  
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kurekebisha uwanja wa Sokoine ili uweze kutumika vizuri wakati wa sherehe za miaka 37 ya CCM.

No comments:

Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma

Na Mwandishi wa OTR Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya mazungumzo na  Fitch Ratings Ltd  amb...