Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, (NHC) Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na waandishi wa habari. Shirika la Nyumba la Taifa kwa kushirikiana na Wakala wa Utafiti wa
Vifaa Bora vya Ujenzi (NHBRA) iliyo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, pamoja na VETA mmetoa mafunzo kwa wataalam wapatao 50, wawili kutoka kila Mkoa ambao baadae watatumika kutoa
mafunzo kwa vijana katika Halmashauri za
Wilaya na Miji kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2014. Mafunzo hayo yanahusu namna ya kutumia
mashine hizo na kutambua udongo unaofaa kutengenezea matofali na namna ya kujenga
kutumia hayo matofali.
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika eneo la mradi Chamazi, Dar es Salaam, Mradi huu ni mali ya wapangaji walioondolewa katika bomoa bomoa ya utanuzi wa Bandari eneo la Keko na Kigamboni wakaamua kuunda umoja wa wamiliki wa nyumba za gharama nafuu eneo la Chamazi ukiitwa Federation.






No comments:
Post a Comment