Tuesday, January 28, 2014

MCD KUZIKWA KIISLAM KESHO SAA 7 MCHANA

 ALIYEKUWA mpiga tumba wa Twanga Pepeta Soud Mohamed 'MCD' aliyefariki jana usiku, atazikwa kesho saa 7 mchana Moshi mjini.
Kwa mujibu wa kiongozi wa Twanga, Luizer Mbutu mazishi ya MCD ilikuwa yafanyike leo saa 10 lakini familia ikakubali kusogeza mbele ili wafanyakazi wenzie pamoja na marafiki wa marehemu waweze kuwahi mazishi hayo.
Msafara wa wasanii wa Twanga, wawakilishi wa bendi zingine, wadau na marafiki, utaondoka Dar es Salaam leo saa 4 usiku kuelekea Moshi.
MCD aliyefariki sekunde chache baada ya kufikishwa  hospitali ya KCMC atazikwa Kiislam, dini aliyoitumikia hadi kufa kwake baada ya kubadili dini mara kadhaa.
Mpiga tumba huyo, kiasi cha kama miaka 13 iliyopita alibadili dini kutoka Uislam na kuwa mkristo hiyo ni kufuatia ndoa yake na…

No comments:

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AMALIZA ZIARA YA SIKU MOJA MKOANI MBEYA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), leo ameondoka Mkoani Mbeya baada ya kukamilisha zi...