Friday, January 24, 2014

OMARY MJENGA AMKARIBISHA WAZIRI NYALANDU OFISINI KWAKE DUBAI

Mr Omary Mjenga akipata picha ya kumbukumbu na Mh. Lazaro Nyalandu ambaye ni Waziri mpya wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania wakati waziri huyo alipomtembelea bwana Mjenga ofisini kwake Dubai.
Mh. Nyalandu akisisitiza jambo kwa Ndugu Mjenga jinsi ya kuweza kuendeleza sekta ya utalii nchini mwetu wakati alipomtembelea ofisini kwake Dubai
Picha juu na chini ni Waziri wa Utalii na Maliasili Mh. Lazaro Nyalandu akiongea na Mwakilishi wa Tanzania Dubai Mr Omary Mjenga kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kudumisha na kuendeleza utalii nchini mwetu.
Mr. Sajwani (Kushoto) akiongea na Mh. Nyalandu
Picha juu na chini Mh. Nyalandu akiwa na mwenyeji wake Mr. Mjenga (Kulia) wakiongea na Mmoja wa wafanya biashara maarufu katika sekta ya ujenzi wa mahotel na majumba mbali mbali ya biashara Dubai Mr. Husssin Sajwani. Katika maongezi yao Mh. Nyalandu alimkaribisha Mr. Sajwani kuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbali mbali hasa katika Mahoteli na Utalii. Mh. Nyalandu ameondoka leo Dubai baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi.

No comments:

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Ashuhudia Utiaji Saini wa Mikataba ya Ushirikiano Kati ya Tanzania na Angola

Luanda, Angola – 08 Aprili 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , leo ameshuhudia utiaji saini wa mi...