Thursday, January 30, 2014

NAIBU WAZIRI WA MAJI AZURU DAWASA NA DAWASCO

IMG_0417Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi za DAWASA. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Said El Maamry na Kulia ni Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa.IMG_0464Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Said El Maamry.IMG_0480Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akizungumza katika mkutano alipotembelea DAWASA.IMG_0560Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala akimwonyesha ripoti ya DAWASCO, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO.IMG_0587Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala akimwonyesha ripoti ya DAWASCO, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO.
………………………………………………………………………..
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala jana alitembelea DAWASA na DAWASCO kuzungumza na uongozi wa taasisi hizo nchini zenye dhamana ya kusimamia huduma za maji katika mkoa wa Dar es Salaam na miji midogo ya Kibaha na Bagamoyo.
Mhe. Makala ametembelea taasisi hizo na kuzungumza na menejimenti na bodi za taasisi hizo ili kufahamu maendeleo na utendaji wa taasisi hizo katika kuleta matumaini ya huduma bora za maji katika mkoa wa Dar es Salaam na mji midogo wa Kibaha na Bagamoyo.
“Tuna chanagamoto ya upatikanaji wa maji, lakini kama Serikali ni jukumu letu kuhakikisha tunalipatia ufumbuzi ”, alisema Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala.
“Hatuna budi kuweka mikakati sahihi na kutekeleza kwa kasi miradi inayoendelea ili wananchi wapate maji na waliopewa dhamana ya usimamiaji watekeleze kwa wakati”, alisema Naibu Waziri.
Pia, Mhe. Makala amedhamiria kutatua tatizo sugu la wizi wa maji na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na akasisitiza wahusika lazima wachukuliwe hatua kali.
Aliongeza suala la upotevu wa maji liwe ni ajenda ya kudumu ili kuhakikisha linakwisha na kuziasa DAWASA na DAWASCO zisiwe chanzo cha matatizo, bali watafute ufumbuzi wa tatizo la maji.
Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa alisema DAWASA imeweka mikakati ya upanuzi wa mitambo na mifumo ya maji, ujenzi wa bwawa la Kidunda na kuthibiti maji yanayopotea kuhakikisha inaboresha huduma zake.
Aidha, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala alisema mikakati waliyojiwekea ni kupunguza madeni wanayodai wateja wake, kufunga mita kwa wateja wote na kuongeza uzalishaji ili kuongeza ufanisi wa mamlaka hiyo.
Hii ni mara ya kwanza tangu Mhe. Makala ateuliwe kuwa Naibu Waziri wa Maji kutembelea taasisi hizo zinazotoa huduma ya maji jijini Dar miji midogo wa Kibaha na Bagamoyos.
Ziara hiyo itaendelea kwa Naibu Waziri wa Maji kutembelea miradi ya maji ya Ruvu Chini na Juu na maeneo ya Segerea na Ubungo.

No comments: