Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(kushoto) akimkabidhi Mshindi wa promosheni ya Timka na Bodaboda, Bw.Wiston Urio hundi yenye thamani ya shilingi Milioni ishirini(20,000,000) baada ya kuibuka mshindi wa mwezi Disemba. Ili kushiriki mteja promosheni hiyo mteja wa Vodacom hutuma neno Promo kwenda 15544.





Aliyetimka na Mil. 20 za Vodacom akabidhiwa kitita chake
•Ni fundi viyoyozi mkazi wa Mbezi Beach
Dar es Salaam Januari 21, 2014 … Hatimae ndoto za fundi viyoyozi yatimia mara baada ya kukabidhiwa kitita chake cha shilingi Milioni 20 alizojishindia kupitia promosheni ya ”Timka na bodaboda”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania huku zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kuisha kwa Promosheni hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo,Bw.Matina Nkurlu amebainisha kuwa hapo awali mshindi huyo na jana ndio tunamkabidhi fedha zake rasmi.
“jana tunamkabidhi mshindi wetu wa Milioni ishirini fedha zake, kama mtakumbuka mara ya mwisho tuliwasiliana nae kwa njia ya simu akiwa mapumzikoni huko kwa Moshi wakati wa sikukuu.
Tumeshuhudia tangu kuanza kwa promosheni hii watu wamekuwa wakishinda pikipiki na fedha taslimu ambazo zimekuwa zikiwasaidia kuboresha maisha yao kwa wale wengi waliojishindia.” Alisema Nkurlu.
Nkurlu aliongeza kuwa “wakati tukikaribia ukingoni, promosheni hii imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na ukweli kwamba wateja wetu wamenufaika kwa kiasi kikubwa na hicho ndio cha msingi. Siku zote tunahakikisha kuja na huduma pamoja na ofa ambazo sio tu kukidhi haja ya mawasiliano bali pia kuwanufaisha au kuboresha maisha ya wateja wetu”.
“Promosheni nzima ilikuwa na jumla ya pikipiki 430 hadi kufikia sasa tumetoa zaidi ya Bodaboda 400 na zimebaki pikipiki 30 pekee na jumla ya fedha taslimu ambazo tumetoa hadi sasa ni Tsh. Milioni 260 kutoka katika milioni 330 hivyo tumebakiwa na milioni 70 ambazo bado zinasubiri washindi”, alisema Nkurlu na kuongeza kuwa “Katika Milioni 70 hizo tunamsubiri Mshindi wa droo kubwa atakaejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 30 siku ya jumatatu tarehe 27 ya januari,kwa hiyo natoa wito kwa wateja wetu na watanzania kwa ujumla kushiriki ipasavyo na kuweza kuondoka na kitita hicho.
Akizungumzia kuhusu ushindi wake wa kitita cha Shilingi Milioni 20 katika promosheni hiyo, Bw.Wiston Urio amesema kuwa siku zote amekuwa akiamini kuwa ipo siku atajikwamua katika maisha yake kwa kujiajiri hivyo kwa yeye kushinda fedha hizo ni hatua kubwa katika kuboresha maisha yake.
“Nimekuwa mshiriki Mkubwa sana katika Promosheni hii na siku zote niliamini ipo siku nitashinda na ndivyo ilivyotokea siku ambapo nilikuwa kijijini kwetu moshi katika mapumziko ndipo nilipopigiwa simu na kuambiwa kuwa mimi ni mshindi wa milioni 20, ilikuwa ni siku ya kipekee sana na ninamshukuru Mungu kwa Baraka hiyo lakini shukurani za kipekee pia ziende kwa mke wangu ambae amekuwa akinihamasisha siku hadi siku kushiriki baada ya yeye kushinda bodaboda.” alisema na Kuongeza.
“Kazi yangu mimi ni fundi viyoyozi ni matarajio yangu kuwa kupitia fedha hii nitaweza kujiendeleza na kuboresha mazingira yangu ya kazi na kujiongezea ujuzi zaidi, ninatoa wito kwa jamii ya Watanzania kuacha kupuuzia au kudharau kushiriki katika promosheni hii,Pia natoa wito kwa watanzania wenzangu kutumia frusa hii ya siku chache zilizobaki kucheza kwa bidii nao waweze kujaribu bahati yao ya kushinda na kuboresha maisha yao” alisema
Ili kujiunga na promosheni ya “Timka na bodaboda”wateja wanatakiwa kuandika neno PROMO na kutuma kwenda nambari 15544.
No comments:
Post a Comment