Wednesday, January 29, 2014

DROO KUBWA YA MILIONI 50/- YA MIMI NI BINGWA YAKARIBIA‏


Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akisisitiza jambo wakati akichezesha droo ya kumi ya promosheni ya Mimi ni Bingwa liyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Bw. Emmanuel Ndaki.
Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akizungumza na mmoja wa washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa aliyepatikana katika droo ya kumi ya promosheni  hiyo iliyochezeshwa jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam na kumtangaza Msemwa George Makuzi kama mshindi wa tiketi mbili za kwenda Old Trafford.

1.     Droo kubwa ya milioni 50/- ya Mimi ni Bingwa yakaribia
2.     Airtel yajipanga kwa droo kubwa ya milioni 50/- ya ‘Mimi ni Bingwa’
WAKATI washindi wa tiketi wa awamu ya kwanza ya promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ wakitarajiwa kuwasili nchini Alhamis, kampuni hiyo ya simu imechezesha droo nyingine na kumchagua mkazi wa jijini Dar es Salaam, Msemwa George Makuzi kuwa mshindi wa tiketi mbili za kwenda Old Trafford katika wiki ya kumi ya droo hiyo.
Akizungumza mara baada ya droo hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema kilele cha promosheni hiyo kinakaribia, ambacho tutashuhudia mshiriki wa ‘Mimi ni Bingwa’akiondoka na kitita cha shilingi milioni 50 katika droo kubwa itakayohusisha kila aliyejisajili katika promosheni hiyo.
“Tukiwa tunafikia kilele cha promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’, nataka niwahakikishie wateja wote wa Airtel kuwa washiriki wapya bado wanakaribishwa kutokana na kuwa mshindi wa pesa taslim ya milioni 50 atapatikana kupitia droo ya bahati nasibu.
“Kupitia droo hii kubwa, ndiyo tutajua ni nani ataondoka na zawadi kubwa ya ‘Mimi ni Bingwa’. Kutokana na vigezo na masharti ya promotion hii, kila namba iliyosajiliwa kwa ajili ya promosheni, hata kama mshiriki alijibu swali moja tu, ataingia katika droo kubwa.
“Hii sasa ni nafasi kwa wateja wa Airtel ambao hajajisajili kwenye promosheni kujisajili kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo, na unaweza kuwa mshindi wa zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 au zawadi nyingine za milioni 1 kila siku na milioni 5 kila wiki kwa wiki zilizobaki,” alisema Jane.
Alisema kuwa ‘Mimi ni Bingwa’ imeonyesha mafanikio makubwa kwa kuwa imepokelewa vizuri na wateja waliojisajili kwa wingi na kujikusanyia pointi kwa kujibu maswali mengi yaliyorahisi yanayoulizwa.
Jane aliongeza kuwa Airtel itaendelea kuanzisha promosheni na kampeni mbali mbali zinazolenga kuwazawadia wateja wake pamoja na kuyabadilisha maisha yao na kuwa washiriki mahiri wa kuubadilisha uchumi wa Tanzania. 
Alibainisha kuwa washindi wote wa tiketi za safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford watasafiri kabla ya mwisho wa mwezi wa Februari, huku akiongeza kuwa mkakati ni kuwawezesha washindi kwenda Uingereza katika awamu tatu tofauti.
Katika droo hiyo ya wiki ya kumi, Bi Hawa Mohammed Hussein kutoka Tanga na Godlove William Kayonga kutoka Mara walijishindia shilingi milioni 5 kila mmoja na washindi wengine 12 kujinyakulia shilingi milioni 1 kila mmoja.
Washindi wengine wa tiketi za ‘Mimi ni Bingwa’ ni pamoja na Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa, Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mtendaji wa kijiji cha Nang’olo wilayani Kilwa – mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro in Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini  Dar es Salaam na Salma Farid Mughery kutoka Dar es Salaam.

No comments: