Wednesday, August 18, 2010

Meryl na Yacob nusura wachapane makonde

JUMBA la Big Brother Africa All States jana iligeuka uwanja wa vita baada ya Meryl na Yacob kuzozana kwa maneno makali kabla ya washiriki wenzao hawajaamua kuwaingilia na kumtaka Yacob amuombe msamaha Meryl.

Yacob ambaye bila woga na mbele ya Mwisho ambaye inasemeka ana uhusiano na Meryl alisikika akisema kuwa mshiriki huyo alitaka kufanya mapenzi na Munya, kitu ambacho kilimkasirisha.

Yacob ambaye awali alilizungumza suala hilo alipokuwa na Kaone na Uti, alidai kuwa Munya alimwacha na kumchukua Tatiana. Meryl alikasirika na kumfuata Yacob.

Mshiriki huyo alisikika akimweleza Yacob kuwa ana uhusiano na watu wengi sana kumshinda yeye hivyo ana uwezo wa kuwaweka nyuma yake na kuwabeba, pia ameshacheza sana na wanaume, hivyo hawezi kumweleza chochote.

Maneno hayo yaliwafanya washiriki wengine kubaki kimya. Baadaye Sheila aliamua kumuuliza swali Yacob, "Hiyo ni tabia yake kuwataka wanaume wa aina yoyote?". Imeandaliwa na Herieth Makwetta.

No comments:

Dkt. Salem Al-Junaibi na Ujumbe wake Awasili nchini kwa Ziara ya Kibiashara

Mwenyekiti wa Chama cha Biashara na Viwanda cha Oman Dkt. Salem Al-Junaibi (Mb) na ujumbe wa Wafanyabiashara wa Oman, amewasili nchini leo, ...