Friday, August 27, 2010

Kenya waidhinisha katiba mpya


Mbwembwe za kijeshi
Rais Mwai Kibaki akiapa.
Mashirika ya haki za binadamu yameilaumu serikali ya Kenya kwa kumruhusu Rais Omar Hassan al-Bashir kuitembelea Kenya ambako atahudhuria sherehe ya nchi hiyo ya kuidhinisha katiba mpya.Kiongozi huyo anatakiwa na Mahakama ya Kimataifa (ICC) kwa mashtaka 10 ya uhalifu, ikiwemo uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari yanayodaiwa kufanyika huko Darfur.

Yeye ni kiongozi wa kwanza aliye madarakani kutuhumiwa na mahakama hiyo ya the Hague. Kenya ni moja ya nchi zilizotia saini mkataba wa mahakama ya ICC ujulikanao kama sheria ya Rome unaoitaka kisheria kumkamata na kumkabidhi kwa mahakama hiyo.

Hata hivyo, uamuzi wa mara mbili uliofanywa na Umoja wa Afrika, uliwaamuru wanachama wake wasimkamate Rais huyo wa Sudan, hata hivyo ulikosea tu kusema kama kuna hatua itakayochukuliwa dhidi ya nchi yoyote itakayokiuka maagizo hayo na kutii amri ya ICC.

Shirika rasmi la habari nchini Sudan (SUNA) limesema katika taarifa fupi kuwa Rais Bashir atasafiri kwenda Nairobi akifuatana na mshauri wake Mustafa Ismail, waziri wa mashauri ya kigeni Ali Karti na mkurugenzi mtendaji wa idara ya ujasusi Muhammad Atta Al-Mawla.

Hii ni ziara yake ya pili katika moja ya nchi wanachama zilizotia saini mkataba wa Rome baada ya kuzuru Chad mwezi uliopita. Licha ya ziara hiyo alipuuza mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa kilele wa nchi wanachama wa IGAD mjini Nairobi mwaka huu.

Shirika la Human Rights Watch limesema kuwa ziara yake itaweka doa sherehe za kuidhinisha katiba iliyosubiriwa kwa hamu kwa kumpokea kiongozi huyo.source BBC.

No comments: