Tuesday, August 31, 2010

Pingamizi la Chadema latinga kwa JK


Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akiwa ameshika nakala ya pingamizi dhidi ya mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, wakidai mgombea huyo amekiuka kanuni za sheria ya gharama za uchaguzi baada ya kuiwasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa jana jijini Dar es Salaam. Picha na Zacharia Osanga

**********************************************************************
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeteketeza azma yake ya kumwekea pingamizi mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa zimeeleza kuwa chama hicho kiliwasilisha pingamizi hilo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini jana saa 7:30 mchana.

Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika, ndiye aliyewasilisha pingamizi hilo.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa alipoulizwa hakutaka kukubali au kukataa kuliona pingamizi hilo na akasema atazungumzia suala hilo leo.

Awali Chadema ilipanga kuweka pingamizi hilo la kutaka Kikwete azuiwe kugombea urais, Agosti 27 mwaka huu, lakini, ilisitisha kwa kile ilichoeleza kuwa inasubiri mambo mengi zaidi ambayo wangeyaingiza kwenye pingamizi hilo.

Chama hicho awali kilitaka kuweka pingamizi hilo kwa kile kilichoeleza kuwa Rais Kikwete amekiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa kutangaza nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi kwenye kampeni.

"Tulishindwa kupeleka pingamizi hilo jana kwa sababu tumesikia kwamba huku anakoendelea na kampeni zake, mgombea huyo ameendelea kufanya makosa mengine ambayo tutataka tuyaingize kwenye pingamizi hilo," alisema Mnyika mwishoni mwa wiki. Habari hii imeandikwa na Geofrey Nyang’oro. SOURCE: MWANANCHI.

1 comment:

emu-three said...

Mhh, lakini hapo napo kuna hoja inayohitaji udadafu wa hali ya juu, kumbuka `alisema, sina pesa za kuongeza,...' mara pesa zina-ahidiwa kipindi cha uchaguzi...'
Lakini najua wote wanajua nini wanakifanya, sisi yetu macho, na masikio, mwisho wa siku kura zetu zitaamua