Thursday, August 05, 2010

Mambo ya Polisi na mihanjo yao


Mkuu wa Wilaya ya Chato Bi. Khadija Nyembo akikagua gwaride maalum lililoandaliwa na askari wa Wilaya hiyo kwa ajili ya kumkaribisha Kamishna wa Polisi anayeshughulikia Operesheni Paul Chagonja wakati wa ziara yake ya ukaguzi Mkoani Kagera.

Askari wa Wilaya ya Muleba wakiwa wamejipanga katika mtindo wa kuhami Kituo wakati wanaonyesha zoezi hilo kwa Kamishna wa Operesheni, Paul Chagonja katika ziara ya ukaguzi wa maeneo mbalimbali ya Polisi Mkoani Kagera.

Kamishna wa Operesheni, Paul Chagonja akisalimiana na wanakijiji wa Kagoma, Wilayani Muleba, Mkoani Kagera mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa uhamasihaji wa Ulinzi Shirikishi kiujijini hapo.

4 comments:

emu-three said...

Hivi ile sera ya mujibu wa sheria imefia wapi, manake naona wafanyakazi wengi maofisini ni nyolonyolo, na machana machips nk, wangepitia jeshi kidogo ingekuwa mambo chap chap, sio unafika ofisini mtu anapaka lips, anaonge na rafiki yake...hajali! Na hata kula ungekuwa tayari kula chochote hata chps dume!

Unknown said...

Sera ya mujibu wa sheria ndio ipi hiyo mkuu? Ni ya mwaka gani na inasemaje?

Anonymous said...

Aisee wewe mkuu ulizaliwa lini, sera hiyo ilikuwa ikisema ukimaliza kidato cha sita, au umemaliza kozi ya ualimu , udakitari nk, unatakiwa ulitumikie jeshi mwaka mmoja tu. Miezi ya kuhenya, na miezi sita ya kujenga taifa, hebu dada Yasinta upo, mmmh, kalala, angetusaidia hili, kama hakujongo!

emu-three said...

Mkuu imejiweka Anonymous hapo juu, sijataka kujificha ila ndiye mimi, ninukuu
emu-three