Wednesday, August 04, 2010

Wakenya wajitokeza kwa wingi kura ya katiba


Kenya's Prime Minister Raila Amollo Odinga casts his ballot on August 4, 2010 at Old Kibera Primary School where he went to cast his vote in the ongoing constitutional referendum. Kenyans voted Wednesday on a proposed constitution to make their institutions more democratic amid tight security aimed at preventing a repeat of deadly post-election violence in 2007-8. AFP / PHOTO

**************************************************************************************************
WANANCHI wa Kenya, jana walijitokeza kwa wingi kupiga kura ya maoni (maamuzi) itakayoamua kama nchi hiyo iwe au isiwe na katiba mpya.

Kwa muda wa miaka 20 sasa, kumekuwepo na shikinizo la kutaka kuundwa kwa katiba mpya ili kukidhi mahitaji ya kizazi kipya nchini Kenya, hasa kwa kuzingatia kuwa katiba ya sasa iliundwa mara tu baada ya uhuru wa nchi hiyo.

Kuanzia saa kumi za usiku wa kuamkia jana tayari kulikuwa na mistari mirefu ya wapigakura katika vituo vya kupigia kura, vya maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi.

Wakenya 12,470, 443 waliojiandikisha kupiga kura, wanatarajiwa kubadilisha historia ya nchi hiyo ikiwa watapiga kura ya ndio kutaka mabadiliko ya katiba.

Kenya nzima ina vituo vya kupigia kura 27,000 na ina majimbo 210.

Ikiwa zaidi ya asilimia 50 ya wapigakura watasema ndio, ina maana ya kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa katika muundo mzima wa serikali na uendeshaji wake.

Rais Mwai Kibaki, aliwataka Wakenya kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

"Kura hii si ya Kibaki, ni kura yenu nyinyi Wakenya kwa maisha yenu," alisema kiongozi huyo wa Kenya.

No comments: