Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (wa pili kulia) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika leo huko Ubungo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Ethur Mwakapugi na kushoto kwa waziri ni Meneja Mkuu wa PanAfrican Energy (T) Ltd Pierre Raillard.
Mfanyakazi wa PanAfrican Energy (T) LTD ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akimuonyesha Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) jinsi ya kuweka gesi katika gari maalum wakati wa uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika leo huko Ubungo jijini Dar es Salaam. Aliyesimama kulia kwa waziri ni Meneja Mkuu wa PanAfrican Energy (T) Ltd Pierre Raillard.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kulia) akimsikiliza mkazi wa Ubungo Maziwa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kuhusiana na maombi yao ya kulipwa fidia ili waweze kahama eneo hilo na kupisha ujenzi wa mitambo kupeleka gesi majumbani, kwenye taasisi na kwenye magari. Waziri Ngeleja alifika katika eneo hilo leo kwa ajili ya uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Yona Killagane wakati wa uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliopo Ubungo jijini Dar es Salaam.Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Comments