CCM yashinda Biharamulo

CHAMA cha CCM hatimaye kimeshinda uchaguzi wa jimbo la Biharamulo Magharibi na kukibwaga chama pinzani cha Chadema kwa kra si zaidi ya 1,000.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi Zuberi Mbyana alisema kuwa CCM wameibuka washindi kwa tofauti ya kura 861 baada ya kupata kura 17561 dhidi ya 16,700 wakati chama cha TLP kikiambulia kura 198.

Alisema katika uchaguzi huo jumla ya watu 87,188 walijiandikisha kupiga kura lakini waliopiga kura walikuwa ni 35, 338 hivyo kura halili zilikuwa ni 35,459 na kura zilizoharibika 879.

Wakati msimamizi akitangaza matokeo hayo mkurugenzi wa oganaisheni na mafunzo Benson Kigaila naye alikuwa akiwatangazia wanachama wake kuwa wao bado wanaamini matokeo yao kuwa wameibuka washindi lakini msimamizi ameamua kuwasaidia CCM kwa kutangaza matokeo wameshinda.

Kila mfuasi wa chama alikuwa akishangilia matokeo yake na kujinadi kuwa kashinda hatua ambayo ilivuta mvutano kwa viongozi wa vyama hivyo na kulazimika kuhakiki matokeo yote kwa kupitia kata zote nane wakiwa mbele ya msimamizi wa uchaguzi. Imendaliwa na Fredrick Katulanda.

Comments