Monday, October 13, 2008

Serikali yalifungia Mwanahalisi

SERIKALI imelifungia gazeti la Mwanahalisi linalochapishwa na Kampuni ya Hali Halisi Publisher, kwa kwa madai ya kuandika habari za uchochezi.

Uamuzi huo ulitangazwa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Kapteni George Mkuchika akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika, serikali imeamua kulifungia gazeti hilo kwa muda wa miezi mitatu kutokana na wamiliki pamoja na mhariri wake kukataa kubadili mtindo wa kuandika habari za serikali na viongozi wakuu.

Alisema Gazeti hilo limekuwa likiandika habari za uchochezi mara kwa mara bila kujali maadili ya kazi yake na kudai kuwa ofisi yake imekuwa ikilionya mara kwa mara bila ya mafanikio.

“Ofisi yangu imeshamwita Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali halisi na kumuonya zaidi ya mara tatu lakini hakuna mabadiliko yoyote kutoka katika gazeti hilo," alisema Mkuchika.
Waziri Mkuchika alisema uamuzi huo unafuatia gazeti hilo katika toleo lake namba 118 la Oktoba 8, 2008 kuandia habari yenye kichwa, “Njama za kung’oa Kikwete zafichuka-Mwanaye Ridhwani atumika –Watuhumiwa Ufisadi wajipanga” makala ambayo Mkuchika alidai kuwa inavunja sheria ya magazeti ya mwaka 1976 kifungu cha (31) (1), kifungu kidogo (d) na (e) na kifungu cha (32) (1) kifungu kidogo (c).imeandikwa na Geofrey Nyang'oro na Festo Polea

No comments: