Friday, October 03, 2008

Dada wa wangwe awaka



MALUMBANO baina ya ndugu wa aliyekuwa mbunge wa Tarime kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Marehemu Chacha Wangwe, yamezidi kupamba moto baada ya dada wa mbunge huyo kuibuka na kumkana mke mdogo, Doto Mohamed kuwa hatambuliki kwenye ukoo.

Kuibuka kwa dada wa mbunge huyo, Mary Zakayo Wangwe kumekuja siku mbili baada ya mke Dotto, ambaye alidai kuwa ndiye aliyeshirikiana na Wangwe hadi kupata ubunge, kupinga madai ya mke mwingine mdogo kuwa Chadema imeitelekeza familia ya marehemu, akisema kuwa ni mapema mno kuzungumzia hilo.

Mariam alikuwa wa kwanza katika malumbano hayo baada ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari wiki iliyopita na kuzungumzia mambo mengi kuhusu utata wa kifo cha mbunge huyo akilitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi zaidi, lakini akamwaga lawama kwa Chadema, jambo ambalo limezua malumbano baina ya wake hao na dhidi ya viongozi wa chama hicho, hasa katibu mkuu, Wilbroad Slaa.

Akizungumza na gazeti hili jana kijijini Kemakorere, dada huyo, Mary Zakayo Wangwe alisema kuwa Dotto Mohamed si mke halali wa Marehemu Wangwe kwa kuwa walishatengana na kwamba aliwahi kumshitaki Ustawi wa Jamii akidai apewe mali, lakini akashindwa katika kesi hiyo.

No comments: