Wednesday, September 03, 2008

Sabato Masalia watimuliwa tena uwanja wa ndege


Polisi yatoa onyo la mwisho kwa Wasabato Masalia

KUNDI la waumini wa Dhehebu la Waadventista Wasabato Masalia, kwa mara ya tatu limesambaratishwa na askari wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kurudi tena uwanjani hapo huku wakiwa wameongezeka idadi yao kutoka 17 hadi kufikia 51.

Wasabato hao masalia, walifika katika uwanja huo mnamo saa 2:00 asubuhi huku wakiwa na mabegi yao tayari kwa safari wakisema: "Bwana alikuwa amewaambia tena kuwa jana ilikuwa ndio siku ya kuondoka na kuelekea nchi za Ulaya kuhubiri injili."
Na Furaha Kijingo

1 comment:

Anonymous said...

Hii kali!

MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. PHILIP MPANGO AONGOZA KIKAO CHA 15 CHA KAMATI YA PAMOJA YA MASUALA YA MUUNGANO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, ameongoza Kikao cha 15 cha Kamati ya Pamoja kati ya Serikali ya ...