Sunday, September 21, 2008

Bomoa bomoa ya kikatili Magomeni




FAMILIA sita zimekosa sehemu ya kuisha baada ya watu wanaodai kununua nyumba ya urithi ya watoto zaidi ya 10 wa marehemu Yussuf Mbonde iliyo Magomeni Mwembechai kubomoa nyumba hiyo kwa kutumia greda huku wakilindwa na vijana wa kukodi maarufu kama mabaunsa pamoja na usimamizi wa polisi waliokuwa na silaha.

Bomoabomoa hiyo ilitokea jana majira saa 9:00 alasiri baada ya uvamizi huo kutokea na kusambaratisha nyumba na vitu vyote vilivyokuwemo ndani.

Mwananchi ilifika eneo hilo mara baada ya tukio hilo na kuwakuta wanafamilia hao wakilia kwa uchungu huku wakilalamikia kitendo hicho ambacho wamekiita ni cha ukatili. habari zaidi soma Mwananchi.Habari yote hii imendikwa na Salim Said ambaye pia kapiga picha zote.

No comments:

MAKATIBU WAKUU WAKAGUA AICC MAANDALIZI YA MWISHO MKUTANO WA IPU, ARUSHA

Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Kamati ya Wataalamu ya Maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamefan...