Mambo NMB sasa mswano




WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB jana walirejea kazini na kuendelea kutoa huduma baada ya kubatilishwa kwa mgomo ulioanza Jumatatu wiki hii, huku kukiwa na kasoro kadhaa katika huduma ambazo zililalamikiwa na wateja wa benki hiyo.Katika tawi la Bank House kulikuwa na msururu mrefu wa wateja walio kuwa wamejipanga kwenye mstari wakisubiri kupatiwa huduma ambayo ilisitishwa tangu Jumatatu, huku mashine za kutolea fedha 'ATM' zikiwa hazifanyi kazi.Kwa mujibu wa wateja waliokuwapo maeneo hayo, mashine hizo zilikuwa hazifanyi kazi tangu walipofika asubuhi na kwamba, walipowasiliana na uongozi waliwaambia hawajui tatizo litatatuliwa saa ngapi.Lakini ilipofika saa 4:00 asubuhi baadhi ya ATM za makao makuu ya benki hiyo, zilianza kufanya kazi kwa kusuasua na baada ya muda zilirejea katika hali yake ya kawaida na watu wakaanza kuchukua fedha.Habari Kwa Hisani Ya Mzee Wa Sumo

Comments