MTANZANIA aliyekamatwa namakachero wa Marekani kwa kuhusishwa na ugaidi, Suleiman Abdallah Salim (Morris), amerudishwa Zanzibar juzi na Shirika la Msalaba Mwekundu kutoka Afghanistan baada ya kubainika kwamba si gaidi.
Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwao maeneo ya Mombasa, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, huku akinekana mchovu, alisema alikamatwa na makachero wa FBI nchini Somali mwaka 2003 akiwa katika shughuli zake za kibiashara na kuingizwa katika gari bila ya kufahamu anapopelekwa.
Akielezea mkasa uliomkuta akiwa eneo la Abusasu, Mjini Mogadishu alisema baada ya kukamatwa na kuingizwa katika gari hilo huku akipata kipigo kutoka kwa maafisa
hao alisafirishwa hadi Nairobi, Kenya na kutakiwa apeleke mtu wa kudhamani, lakini aliwaambia kuwa yeye ni Mtanzania na hana kwamba ndugu yeyote jijini humo.
“Walinambia mimi ni Msomali nilikataa nikiwaambia kuwa ni Mtanzania. Kisha wakasema ni Myemen nikasema ni Mtanzania walipoona nasema kiswahili wakananimbia mlete ndugu yako akuwekee dhamana, nikawaambia sina jamaa Nairobi mimi
kwetu ni Tanzania,” alisimulia Salim.
Alisema baadae alirejeshwa tena Somali na kuwekwa kwenye kambi ya jeshi na kila mara alikuwa akiulizwa maswali huku akipata kipigo wakati akijibu maswali yao.
Alisema baadhi ya maswali aliyoulizwa yalihusu kama anawafahamu Khalfan, Marwan na Fahad na kutakiwa kusema hao ni akina
nani kwake na kwamaba aliwajibu kuwa anawafahamu kwa kuwa ni rafiki zake wa karibu aliokuwa akifanya nao kazi ya uvuvi maeneoo ya Mombasa kabla ya kwenda Somali. Habari ya Salma Said, Zanzibar.
Comments