WANAUME WAASWA KUACHA TABIA YA KUWANYANYASA WANAWAKE NA KUWAACHIA MAJUKUMU YA KUZIHUDUMIA FAMILIA ZAO.



 

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

KATIKA kuelekea siku ya Wanawake Duniani, Baafha ya Wanawake Mkoani Kigoma Wamewaomba Wanaume Mkoani humo kuacha tabia ya kuwanyanyasa wanawake kwa kuwaachia majukumu ya kuzihudumia familia zao, hali inayosababisha Watoto wengi kukosa elimu na wanawake kushindwa kufikia Malengo yao ya kujikomboa na umasikini.

Akizungumza na Globu ya Jamii ofisini kwake jana, katibu wa umoja wa Wanawake Mkoani Kigoma , Salome Luhinguranya alisema kumekuwa na tabia ya Wanaume wengi kukimbia familia zao na kuwaachia mzigo wa malezi na kusomesha watoto wanawake wao hali inayo wapelekea wanawake wengi kishindwa kufanikiwa katika biashara zao kuyokana na Mzigo mkubwa unao Walemea.

Luhinguranya alisema Watoto wengi wamekuwa wakikosa elimu Mkoani humo kutokana na matatizo ya Wanajme wengi kuwatelekeza wake zao na familia zao na kwenda kuoa wake wengine hali inayo wapelekea Wanawake kushindwa kuhudumia familia zao kutokana na ufinyo wa mitaji waliyo nayo.

"Kauli mbiu ya Mwaka huu katika maadhimisho ni Tanzania ya Viwanda wanawake ni msingi wa mabadiliko Kiuchumi,kuelekea. Mkoa wa kigoma wanawake wengi wanajishughulisha katika Shughuli mbali mbali na Wengine ni wafanya kazi ,
 
UWT Mkoa imewahamasisha kuingia kwenye ujasiliamali huo na wanaume wengi wamekuwa Wakiwarudisha Nyuma kutokana na mizigo wanayo waachia , niwaombe wanaume kuepukana na fikra mgando ya kuwanyanyasa wanawake pindi wanapo jishughulisha kwa kuwaachia kulea familia ,
 
Baba ni kichwa katika familia wanatakiwa kutafuta fedha na kuwasaidia wanawake kulea familia zao ilikuwasaidia watoto kupata elimu na malezi bora", alisema Katibu wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa kigoma.

Mipango ya umoja wa UWT ni kuwashauri wanawake na kufanya makongamano ya kuelimishana jinsi ya kufanya biashara na kuunda vikundi vya kununua hisa na kupata mikopo ambayo haina riba ilikuweza kuepukana na umasikini na suala hili limefanikiwa kwa mkoa wa Kigoma zaidi ya Wanaume wengi ndio wamekuwa wakiwarudisha nyuma katika sula la kuinuka kiuchumi.


Kwa upande wake Sadda Msomali ni mfanya biashara wa Samaki soko la Buzebazeba Mkoani humo ni mama wa Watoto saba alisema kwaupande baada ya kuanza biashara hiyo Mume wake alimuacha na watoto wake kwa madai kiwa dini yake hairuhusu mwanamke kufanya biashara, mwanamke ni mtu anaetakiwa kukaa ndani na kulea watoto.

Alisema baada ya kuona Maisha yamekuwa magumu katika familia yake alimuomba Mumewake aweze kufanya biashara ilikulea watoto wake, mume wake alimwambia endapo ataanza biashara hiyo atatakiwa kumpa taraka na amrudishe nyumbani kwao ndipo alipo muacha na watoto wake saba ambao watano anatakiwa kulipa ada zao na kutafuta Chakula chao hali ambayo inafanya maisha kuwa magumu kwake.

Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa kigoma , Zilpa Kisonzela alisema katika Mkoa Wakihoma kuna jitahada nyingi za kujikwamua na uchumi, wanawake wengi wamekuwa wakitumia fursa hizo katika kuzalisha Sabuni za Magadi , kutengeneza unga wa muhogo na kununua mazao ya ziwa Tqnganyika na kuyaongezea uthamani na kupeleka kuuza katika Nchi jirani za burundi na Congo Drc.

Alisema dhumuni hilo limefanikiwa na wafanya biashara wakubwa Wa vitenge na biashara mbalimbali Mkoani humo ni wanawake , kumekuwa na changamoto kubwa kwa Wanaume kuwarudisha nyuma kwa kuwatelekezea familia kutokana na mfumo wa malezi uliopo katika mkoa huo ambao umemuandaa mwanaume kuishi kama mfalme na Wanawake kuwa watafutaji hali inayo pelekea kushindwa kufikia malengo yao.

Aidha Kisonzela aliwataka wanaomu kushirikikana na Wanawake zao katika kulea familia na kujenga uchumi wa familia zao ilikuweza kuepukana na umasikini, endapo mwanaume atatafuta na mwanamke atatafuta itasaidia kujenga uchumi wa familia na kuepukana na malalamiko ya utegemezi

Comments