Wednesday, March 15, 2017

BancABC YAZINDUA AKAUNTI MAALUM NA YA KIPEKEE


 Bi. Joyce Malai Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati wa BancABC, akionyesha bango lililoandikwa Jiongeze Maradufu katika uzinduzi wa akaunti hiyo maalum ya kipekee katika makao makuu ya BancABC jijini Dar es salaam.
 Bi. Upendo Nkini Mkuu wa kitengo cha masoko wa BancABC akizungumza jambo na waandishi wa habari katika uzinduzi wa akaunti maalum ya Jiongeze maradufu. Uzinduzi huo ulifanyika katika makao makuu ya BancABC jijini Dar es salaam.
 Bi. Joyce Malai (kushoto) Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati,  na  Bi. Upendo Nkini Mkuu wa kitengo cha masoko wa BancABC wakionyesha (bidhaa) Akaunti mpya na ya kipekee JIONGEZE MARADUFU iliyozinduliwa na BancABC.
Joyce Malai akitoa ufafanuzi kuhusu akaunti maalum ya Jiongeze Maradufu iliyozinduliwa na BancABC.
JIONGEZE MARADUFU. Pata riba hadi asilimia kumi na sita (16%)kwa mwaka katika amana hii na kujipatia fursa ya kukopa dhidi ya amana yako.

 BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, leo imezindua bidhaa adimu itakayokuwezesha kuvuna riba hadi asilimia 16% kutokana na akiba maalum utakayojiwekea.

Katika hali ya kawaida kama tulivyozoea, amana za muda maalum zimekuwa kivutio kwa wateja wengi wa mabenki. Kwa kuanzia amana hii yenye riba kubwa ni nzuri kuliko kufungua akaunti ya akiba ya kawaida kwani unapata riba nzuri zaidi.

Faida nyingine ni  uhakika wa mapato ya riba na uwezo wa kuamua namna gani ya kuitumia, kukopa au kuweka akiba zaidi, utakavyopenda mwenyewe.

BancABC imechukuwa hatua kubwa zaidi kwa kutoa riba ya asilimia 16%, vilevile utapata riba hii bila ubabaishaji.

Akiongea jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya benki hiyo, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wale wafanyabiashara wa kati. Mama Joyce Malai alisema hakuna tena nafasi nzuri ya kunufaika na huduma za benki kama hii iliyopo sasa.

 “Tunathamini mchango mzuri wa wateja wetu, kwa hiyo kama benki makini kupata ruzuku tunatoa huduma hii ya kipekee kama zawadi maalum”.

Hii haina tofauti ya kupata faida ya biashara hata kabla hujaianza!  Tunaamini tumeileta huduma hii kwa wakati muafaka, katika muda inayohitajika haswa.  Tuna hakika bidhaa hii mpya ya kibenki itawavutia wateja wengi  hasa wale walio makini”, alisema Joyce.

“Riba ya  asilimia16% inayolipwa kabla hujamaliza muda wa kuweka akiba, ni kivutio kikubwa, ambacho kitamfanya mteja ajivue majukumu makubwa ikiwa pamoja na kulipa ada za shule, kodi ya nyumba, usafiri au kuitumia kama mtaji kwenye biashara zingine azipendazo kwa kuchukua mkopo ambao dhamana ni amana yako katika benki hapo kwa hapo.

 “Vile vile nawasihi wale wote ambao hawana akiba na  BancABC kutumia nafasi hii na kufaidika kwa kufungua akaunti na kupata maelezo zaidi juu ya faida ya huduma hii ya kipekee.  BancABC iko makini kukutana na wateja wake ili kujenga misingi ya mafanikio ya pamoja“, alimalizia.
BancABC ipo tayari kutoa huduma hii kwa wateja wake na wasio wateja kuanzia leo   kwa miezi miwil.
Post a Comment