Saturday, March 18, 2017

Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akizungumza katika mkutano na wananchi wa mtaa wa Maweni wakati wa harambee ya kuchangisha ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maweni iliyopo wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema).Meya wa Jiji la Dar,Isaya Mwita akitia saini kitabu cha wageni alipowasili katika shule ya msingi ya Maweni iliyopo Kata ya Mji Mwema wilayani Kigamboni.Anayeshuhudia kuli ni Mkuu wa Shule hiyo,Zuhura Mwaliko na Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo,Kabega Ally.Uongozi wa Shule ya Msingi Maweni ukimtembeza mgeni rasmi kuangalia maeneo ya shule hiyo na changamoto zake.Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) akimuongoza Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita kuzungukia majengo ya shule hiyo kujionea changamoto zake akishirikiana na Mkuu wa shule hiyo,Zuhura Mwaliko.


Post a Comment