Friday, March 31, 2017

JESHI LA POLISI NCHINI LAVUTIWA NA MIKAKATI YA NHC KUBORESHA MAKAZI

Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Itandula Gambalagi akijadiliana jambo na Naibu Kamishna wa Bajeti wa Jeshi la Polisi nchini, Massawe kusiana na taratibu mbalimbali zinazohusu mauzo ya nyumba ni baada ya Shirika la Nyumba kuwasilisha mada kwenye mkutano huo wa Makamanda wa Jeshi la Polisi waliokuwa wakikutana mjini Dodoma. Katika mkutano huo Makamanda hao walivutiwa na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Shirika la Nyumba katika kuhakikisha kunakuwapo makazi bora.
Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Itandula Gambalagi akijadiliana jambo na Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini, Silla ambaye pia alikuwa Katibu wa Kikao hicho kusiana na taratibu mbalimbali zinazohusu mauzo ya nyumba ni baada ya Shirika la Nyumba kuwasilisha mada kwenye mkutano huo wa Makamanda wa Jeshi la Polisi waliokuwa wakikutana mjini Dodoma.
Afisa Mauzo Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Sophia Mwema akijadiliana jambo na Kamishna wa Polisi, Ahmed Msangi ambaye pia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza hiyo ilikuwa mjini Dodoma jana.
 Makamanda wa Jeshi la Polisi nchi wakifuatilia kwa kina wasilisho lililikuwa likifanywa na Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Itandula Gambalagi .
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Jenerali Ernest Mangu na Wakuu wenzake wakifuatilia wasilisho hilo la Shirika la Nyumba la Taifa.
 Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Itandula Gambalagi akiwasilisha mada kwenya mkutano wa viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi nchini uliofanyika mjini Dodoma.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akiuliza swali katika mkutano huo.

No comments: