NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI AKUTANA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI NA UJUMBE WAKE JIJINI DAR ES SALAAM
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha Balozi wa Ujerumani Nchini, Egon Kochanke na ujumbe wake, wawekezaji kutoka Denmark na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha mbolea Kilwa mkoani Lindi.
Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Sehemu ya ujumbe kutoka Ujerumani na wawekezaji kutoka Denmark wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo akifafanua jambo katika kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akisalimiana na Balozi wa Ujerumani Nchini, Egon Kochanke (kushoto) kabla ya kuanza kwa kikao hicho.
Comments