Thursday, March 23, 2017

WANANCHI NAWAOMBA MYAKUBALI MAAMUZI YALIYOFANYWA NA RAIS WETU-NAPE NNAUYE

Aliyekuwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam leo
 
 Aliyekuwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akifafanua jambo kwa msisito alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam leo
Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye alipokuwa akizungumza nao.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na mbunge wa Mtama Nape Mosses Nnauye amewataka Watanzania kukubaliana na suala la kusitishwa kwake uteuzi wa cheo hicho baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amemteua Dk Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi hiyo ya Nape.

Akizungumza na waandishi nje ya Hoteli ya Protea leo, Nape amesema wanatakiwa kukubaliana na hali halisi kwani uteuzi uliofanywa huwezi kuukosoa na anashikuru kwa kuweza kupata muda wa kufanya kazi na Rais Magufuli.

“Wanachi mnatakiwa kukubaliana na maamuzi yaliyofanywa na Rais wetu kwani tukumbuke kuwa Tanzania ni kubwa kuliko Nape na maamuzi yaliyofanywa yana tija kubwa sana kwa tasnia ya habari, michezo na wasanii na hampaswi kuanzisha matatizo, Tanzania ni nchi yetu sisi na tujue Nape hawezi kuwa mkubwa kuliko Tanzania,"

Nape amesema kuwa anawashauri watanzania wote kuwa watulivu na zaidi amefurahi kufanya kazi kama Waziri wa habari na amewaomba wana tasnia ya habari ya habari kushirikiana na Waziri Mteule Harrison Mwakyembe kwani ni mwanahabari na pia ni mwanasheria mzuri.

“Nina amini nilitumia akili zangu zote na kwa akili nawashukuru wasanii, waandishi, wanamichezo kwa ushirikiano wenu. Nilipenda kuendelea kufanya kazi nanyi lakini muda wa aliyeniteua umefika, nitawakumbuka sana, ninawapenda sana ila ninawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe na kuendelea kumwamini Rais wetu John Pombe Magufuli kwani ndiye tuliyepewa na mungu, ndiye rais tuliyemchagua,” amesema Nape.

No comments: