WAOMBAJI WA NAFASI YA MKAGUZI MSAIDIZI UHAMIAJI ZAIDI YA 10,000 WAFANYA USAILI WA AWALI UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAAM
Sehemu ya waombaji zaidi ya 10,000 wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi,
Idara ya Uhamiaji wakifanya usaili wa awali wa kuandika ulioandaliwa
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ajili ya kujaza nafasi 70 za
kazi ambazo zinahitajika katika Idara hiyo. Usaili huo uliongozwa na
Maafisa Utumishi wa wizara hiyo, umefanyika Uwanja wa Taifa, jijini
Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja waliofaulu vizuri wataitwa
kwa ajili ya usaili wa mwisho.
Afisa Utumishi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Penina Isamuyo akigawa
makaratasi ya mitihani kwa waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi, Idara
ya Uhamiaji kwa ajili ya kufanya usaili wa awali wa kuandika. Zaidi
ya waombaji 10,000 walifanya usaili huo Uwanja wa Taifa, jijini Dar
es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja watakaofaulu vizuri wataitwa
kwa ajili ya usaili wa mwisho.
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lubert Fransis (kulia)
na Mwanamridu Jumaa wakipanga maboksi kwa ajili ya kuhifadhia makaratasi
ya mitihani ya usaili. Zaidi ya waombaji 10,000 walifanya usaili wa
awali Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki
moja waliofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Lilian Mapfa (kulia) akiwa na Meneja wa Uwanja wa Taifa, Rish
Moses wakati wa usaili wa waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa
Idara ya Uhamiaji. Zaidi ya waombaji 10,000 wamefanya usaili wa awali
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kugombea nafasi 70 zilizotangazwa
na Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Afisa Utumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwanamridu Jumaa
(aliyevaa kiraia) na askari Magereza wakiwa wamebeba maboksi yenye makaratasi
ya mitihani ya usaili iliyofanywa na zaidi ya waombaji 10,000 Uwanja
wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo. Baada ya wiki moja waombaji waliofaulu
vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Lilian Mapfa akisimamia usahihishaji wa mitihani ya usaili ya waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa
Idara ya Uhamiaji inayosahihishwa na Maafisa Utumishi wa wizara na askari
Magereza. Zaidi ya waombaji 10,000 wamefanya usaili wa awali Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kugombea nafasi 70 zilizotangazwa
na Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Lilian Mapfa akisimamia usahihishaji wa mitihani ya usaili
ya waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji
inayosahihishwa na Maafisa Utumishi wa wizara na askari Magereza.
Zaidi ya waombaji 10,000 wamefanya usaili wa awali Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam leo kwa ajili ya kugombea nafasi 70 zilizotangazwa na
Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
PICHA ZOTE NA -KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Comments