Monday, June 30, 2014

Rais Jakaya Kikwete Alipokutana na Wataalamu Watatu wa Utafiti wa Chanjo ya Malaria Kutoka Ifakara Health Institute Mjini Malabo, Equatorial Guinea

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dr Ally Olot, mtafiti wa chanjo ya malaria na kiongozi wa watafiti wa Ifakara Health Institute (IH) I Malabo, Equatorial Guinea) walipomtembelea kwenye makazi yake mjini Malabo ambako Rais alikuwa anahudhuria mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika. Wengine ni Dr. Mwajuma Chemba ambaye ni Mtalaamu mratibu wa tafiti za chanjo ya malaria, na Elizabeth Nyakarungu, Mtaalamu wa maabara, utambuzi wadudu wa malaria
 Rais Kikwete aliwapongeza sana watafiti hao pamoja na taasisi ya IHI kwa kuiletea sifa Tanzania katika fani ya utafiti nje ya nchi.

Watafiti hao wako Equatorial Guinea (EG) kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kutoa msaada wa kitaalamu katika utekelezaji wa mradi wa utafiti wa chanjo ya malaria iitwayo PfSPZ na kuwafunza wenzetu kuhusu maarifa ya fani hii ya utafiti wa chanjo ya malaria. IHI ni shirika la utafiti lenye kufanya tafiti za afya nchini Tanzania lenye uzoefu wa miaka zaidi ya miaka hamsini. Mfano mmoja wa mafanikio yake ni utafiti uliopelekea vyandarua vyenye dawa kutumika kama moja wapo ya njia za kujikinga na malaria nchini Tanzania.

No comments: