Uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia Kidato cha Tano katika shule za Serikali na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2014 watangazwa
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI
Uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia Kidato cha Tano katika shule za Serikali na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2014 umekamilika. Uchaguzi umefanyika kwa kuzingatia takwimu za matokeo ya watahiniwa waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne Tanzania Bara mwaka 2013.
2.0 WATAHINIWA WALIOFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE, MWAKA 2013
Jumla ya watahiniwa 427,679 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2013, wakiwemo wasichana 199,123 sawa na asilimia 46.56 na wavulana 228,556 sawa na asilimia 53.44. Kati yao watahiniwa 404,083 sawa na asilimia 94.48 walifanya mtihani na watahiniwa 23,596 sawa na asilimia5.52 hawakufanya mtihani huo.
2.1 Watahiniwa wa Shule (School Candidates)
Kwa Watahiniwa wa Shule, watahiniwa 367,163 walisajiliwa kufanya mithanikati yao wavulana ni198,099 na wasichana ni 169,064. ambapo watahiniwa 352,614 sawa na asilimia 96.04 walifanya mtihani; kati yao wasichana walikuwa 162,412 sawa na asilimia 96.07 na wavulana 190,202 sawa naasilimia 96.01. Watahiniwa 14,549 sawa na asilimia 3.96 hawakufanya mtihani kwa sababu mbalimbali.
Comments