Viongozi wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao(hayupo pichani) kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Philip Mangula akimkabidhi zawadi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao mara baada ya kumaliza mkutano .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao akionyesha zawadi aliyopewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula mara baada ya kumaliza mkutano baina ya viongozi wawili.
Balozi wa China Nchini Tanzania Lu Youqing akifafanua jambo wakati wa Semina ya Ujamaa iliyohusisha CCM na CPC kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akizungumza wakati wa Semina inayohusu Umuhimu wa Ujamaa na Kukua kwa Uchumi,wengine pichani(kushoto) ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Abdala Bulembo ,Mwakamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Mboni Mhita ,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Ndugu Sixtus Mapunda ,Profesa Max Muya ,na Makwaia wa Kuhenga.
Mr Ma Zhongji kutoka Ubalozi wa China akisaidia kutafsiri wakati wa Semina ya Ujamaa iliyohusisha CCM na CPC iliyofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa kutoka CCM Makao Makuu wakifuatilia kwa makini Semina inayohusu Umuhimu wa Ujamaa katika Kukua kwa Uchumi iliyofanyika katika ukumbi wa Kivukoni,Serena Hotel Dar es Salam.
Mheshimiwa Kingunge Ngombale Mwiru akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Hotel ya Serena jijini Dar Es Salaam na kuwaeleza kuwa Watu wanajenga Ujamaa wenyewe haujengwi na Viongozi peke yao.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukamilika kwa Semina inayohusu Ujamaa iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo Mangula liwaeleza waandishi hao kuwa Ujamaa unatakiwa Ueleweke, Utekelezwe na Uendelezwe, Semina hiyo iliwahusisha vyama vya CCM na CPC kutoka China.
Comments