Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakitoka katika lango la ofisi za Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane tayari kuelekea kisiwani
| Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habariwakiwa katika boti wakielekea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane. |
| Mwandishi wa Habari wa kituo cha TBC 1,Ben Mwaipaja akiwa ameshika jembe lake tayari kwa ajili ya kuchukua matukio. |
| Safari ilikuwa ni ya takribani dakika 15 hadi 20. |
| Hatimaye Watalii hao wa ndani wakafika katika Kisiwa cha Saanane. |
| Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakikaribishwa na Mwongoza Watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Saanane Patricia Mtenga. |
| Safari ya kuelekea katika eneo la kuanzia ziara ya kitalii katika Hifadhi hiyo ikaanza. |
| Baadae Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakapata historia ya Hifadhi hiyo kutoka kwa Muongoza Watalii Fua Hamis. |
| Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa makini maelezo ya mhifadhi Fua Hamis(Hayupo Pichani) |
| Safar ya kutembelea maeneo mbalimbali katika hifadhi hiyo ikaanza. |
| Moja ya eneo ambalo liliwavutia Wahariri hao ni eneo hili ambalo unatazama Taswira ya Ziwa Victoria vyema. |
| Safari iliendelea. |
| Baada ya kupita katika maeneo mbalimbali Safari ya Kurudi ikaanza. |
| Wakati Safari ya kurudi ikiendelea bahati mbaya Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA ,Ibrahim Mussa aliteguka mguu baada ya kukanyaga vibaya jiwe hali iliyopelekea kupatiwa huduma ya kwanza. |
| Baada ya kufikishwa katika eneo la Mapumziko ndiko kukafanyika taratibu za kupelekwa Hosptali kwa ajili ya matibabu zaidi. |
| Hatimaye akapelekwa Hosptali. |
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment