Katibu Itikabu wa NEC,itikadi na Uenezi-CCM, Nape Nnauye Alivyotinga Jimboni Kwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo -Chadema John Mnyika

  Nape akizindua Shina la wakereketwa wacheza bao, tawi la Jumuia ya Wazazi la 770, Kimara, wakati wa ziara hiyo.
Vijana wa Chipukizi wa CCM, wakimvisha skafu Nape alipowasili katika kata hiyo kuanza ziara ya siku moja jana,Juni 15, 2014. Kushoto ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge

   Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Dar es Salaam, Ramadham Madabiba akimlaki Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape  Nnauye alipowasili katika Kata ya Kimara kwa ajili ya ziara ya siku moja kukagua uhai wa Chama katika kata hiyo,jana Juni 15, 2014.
  Nape akisalimia wananchi baada ya kuwasili uwanja wa mkutano wa Kimara TRA, kuhutubia mkutano wa hadhara mwishoni mwa ziara yake ya siku moja katika Kata ya Kimara.
Wananchi  wakimshangilia Nape baada ya kuwasili uwanja wa mkutano wa Kimara TRA
  Madabida akimkaribisha Nape kuhutubia kwenye mkutano huo
Nape akihutubia kwenye mkutano huo, mwishoni mwa ziara yake katika kata ya Kimara
  Wanachama waliopewa kadi kwenye mkutano huo, wakila kiapo.
Wananchi wakiselebuka wakati Nape akicharaza gita na bendi ya Vijana Jazz, baada ya kuwasili uwanja wa mkutano wa Kimara TRA,wakati wa ziara hiyo.
  Nape akimkabidhi kadi ya CCM, Domina Emmanuel, wakati wa mkutano wa hadhara Kimara TRA. Jumla ya wanachama wapya 480 wakiwemo waliohamia CCM wakitoka vyama vya Chadema na CUF walipewa kadi baada ya kujiunga na CC

Comments