Thursday, June 19, 2014

MKE WA RAIS MAMA ALMA KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA OFISI YA TEWO SACCOS-TEMEKE.

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la TEWO Saccos huko Temeke 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi jengo la ofisi ya TEWO Saccos kwa kufungua kitambaa katika sherehe iliyofanyika wilayani Temeke jana Kushoto kwa Mama Salma ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Janneth Masaburi.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti  Ndugu Yusuf Manji kilichotolewa na TEWO Saccos  kwa watu na makampuni mbalimbali yaliyoshiriki katika kuchangia ujenzi wa jengo la TEWO Saccos huko Temeke
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mjoumbe wa Bodi ya TEWO Saccos Mama Catherine John (Bi Nyakomba) wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la Saccos hiyo huko Temeke jana
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea Tuzo maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa TEWO Saccos  Ndugu Sophia Kinega. Mama Salma alipewa Tuzo hiyo kwa ajili ya ushirikiano wake na Saccos hiyo katika kuchangia kwa kiasi kikubwa ujenzi  wa jengo la ofisi ya TEWO Saccos.
  Mwakilishi wa Kampuni ya Mabasi ya Usafiri Dar es Salaam, UDA, Ndugu Simon Bulenganiya akikabidhi  mfano wa hundi ya sh 30,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya TEWO Saccos kwa Mwenyekiti wa Saccos hiyo Ndugu Sophia Kinega wakati wa sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti (Certificate of Appreciation) Ndugu Philomena Marijani, Afisa kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, kilichotolewa na TEWO Saccos kwa ajili ya kuwashukuru watu na Taasisi mbalimbali zilizochangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa ofisi za Saccos hiyo huko Temeke
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia wanachama wa TEWO Saccos, mwana Vicoba na wananchi wa wilaya ya Temeke waliohudhuria sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za TEWO Saccos huko Temeke

No comments: