Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana Aung'uruma Mbulu,Maelfu Wajitokeza

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mbulu na kuwataka kutumia muda mwingi kwenye shughuli za kimaendeleo kwa kushirikiana na serikali. Katibu Mkuu alisisitiza serikali kuchukua hatua za haraka kwa wale wote waliojichukulia mali ya serikali bila utaratibu hasa nyumba za madaktari.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mbulu na kuwaambia vyama vingi vya upinzani vinakufa kwa sababu ya kuwa na sera zisizoaminika kwa Watanzania na ameshukuru kwa Watanzania wengi kuelewa hilo kiasi cha kurejea CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanakijiji cha Bashei ambao walimueleza kuwa wanalima sana kitunguu saumu lakini soko si zuri na kumuomba awasaidie kutafuta soko la kdumu, tatizo jingine ni ucheleweshaji wa kujenga bwawa la maji, Katika ziara hizi za Katibu Mkuu wananchi wamekuwa na imani kubwa na CCM kwa ushirikiano wanaoupata kwani majibu ya maswali yao yanakuwa ya kuridhisha.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Anatory Choya akijibu maswali ya wananchi wa Yaeda Chini ambao wamekuwa wakivamiwa na kufukuzwa kwenye ardhi yao,Mkuu wa Wilaya alisema kwanza walishaweka mipango ya matumizi bora ya ardhi kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji ,pili atafanya jitihada za dhati kuwakamata wale wote wanaofukuza na kunyanyasa wananchi wengine kwenye masuala ya ardhi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu wa shule ya sekondari Yaeda chini.

Comments