Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha balozi mmoja pamoja na wajumbe wanne wa Tume ya Operesheni Tokomeza katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Balozi aliyeapishwa ni Joseph Edward Sokoine ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Wajumbe walioapishwa nia pamoja na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Hamisi Amiri Msumi,Jaji Mstaafu Steven Ernest Ihema,Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo pamoja na katibu wa tume hiyo Bwana Frederick Kapela.



No comments:
Post a Comment