Sunday, November 11, 2012

MANGULA KUWA MAKAMU MWENYEKITI MPYA WA CCM-BARA


DODOMA, TANZANIA
Chama Cha Mapinduzi kimemteua Katibu Mkuu wake mstaafu, Philip Mangula kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara huku kwa Zanzibar akiteuliwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

Uteuzi wa wagombea hao umefanywa na Kikao Cha CC na Kudhinishwa na NEC usiku wa kuamkia leo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema leo mjini Dodoma.

Mangula na Dk. Sheni watapigiwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu, unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Kizota nje kidogo ya mji wa Dodoma.

No comments:

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU ASAFIRI KWA SGR KUELEKEA DODOMA

  Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 30, 2026 amesafiri kwa treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma. ...