HATIMAYE
kile kitendawili cha muda mrefu cha Nani ata twaa taji la Redds Miss
Tanzania 2012, kimeteguliwa usiku wa Novemba 3, 2012, baada ya Mrembo
kutoka Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,
Brigitte Alfred kutwaa taji hilo.
Brigitte
ambaye nyota yake katika mashindano hayo ya urembo nchini ilianza
kung’aa tangu Kitongoji cha Sinza baada ya kutwaa taji la Sinza na Baade
kutwaa Taji la Redds Miss Kinondoni amedhihirisha ukali wake baada ya
kuwabwaga warembo wenzake 29 waliokuwa wakiwania taji hilo kutoka Kanda
mbambali.
Mpinzani
mkubwa wa Brigitte katika shindano hilo alikuwa ni Mrembo kutoka Kanda
ya Ziwa ambaye nae alianza kuwika baada ya kutwaa taji la Redds Mkoa wa
Mara na baade kutwaa taji la Kanda ya Ziwa, Eugene Fabian.
Enagene
alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika shindano hilo kubwa ambalo
Brigitte ameondoka akiendesha gari aina ya NOAH na kitita cha Shilingi
Milioni 8.
Nafasi
ya tatu ilikwende kwa Malkia wa Kitongoji cha Kigamboni City na Miss
Temeke 2012, Edda Sylvesta huku nafasi ya Nne ikichukuliwa na Mrembo wa
Dar Indian Ocean na Kinondoni, Magdalena Roy na nafasi ya Tano ikienda
Kanda ya Ziwa tena kwa Mkoa wa Mwanza, Happyness Daniel.
Brigitte Alfred akipunga mkono kwa furaha mara baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi na kuwabwaga washiriki wenzake 29.
Brigitte Alfred (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Miss Tanzania 2011, Salha Izrael
Mshindi
wa Taji la Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati)
akipunga mkono kwa furaha katika picha ya pamoja na mshindi wa Pili,
Eugene Fabian (kushoto) na Mshindi wa Tatu, Edda Sylvester mara baada ya
warembo hao kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo. Brigitte
anatokea Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni wakati, Eugene
anatoka Mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa huku Edda ni Miss Kigamboni na
Kanda ya Temeke.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatu5 bora ya Redds Miss Tanzania 2012,
kutoka kushoto ni Brigitte Alfred, Eugen Fabian, Happyness Daniel, Edda
Sylvester na Magdalene Roy wakipozi kwa picha.
Washiriki wakicheza show ya ufunguzi wakati wa kuanza kwa shindano hilo.
Wageni
mbalimbali na wadau wa tasnia ya Urembo nchini Tanzania wakifuatilia
shindano hilo kwa umakini ndani ya Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es
Salaam.
Wasanii wa kundi la Ngoma za Asili la Wanne Stars likitoa burudani kwa wageni.
Balozi wa Tanga Beach Resort, Happyness Rweyemamu akijinadi jukwaani na vazi lake la ubunifu.
Mshiriki
Flavian Maeda kutoka Kitongoji cha Kurasini na Kanda ya Temeke jijini
Dar es Salaam akipozi jukwaani na vazi la ubunifu.
Fina Recatus akipita jukwaani na vazi la ubunifu. Fina ni Balozi wa Tanga Beach Resort 2012.
Naomi Jones nae akipita jukwaani na vazi la ubunifu
Mrembo wa Dar Indian Ocean na Kinondoni, Kudra Lupato nae alikatiza jukwaani
Brigitte akipozi na vazi lake la Ubunifu
Msanii
kutoka THT Rachel nae alipata fursa ya kuonesha kipaji chake na
kudhihirisha wazi kuwa yeye ni Mrithi wa Ray C kwa sauti na kiuno Bila
mfupa.
Japokuwa ni ufukweni lakini chini walivaa hivi, maana shindano la Dunia ndivyo inavyokuwa
Warembo mbalimbali wa Redd's Miss Tanzania 2012 wakionekana Jukwaani katika vazi la ufukweni.
Warembo mbalimbali wa Redd's Miss Tanzania 2012 wakionekana Jukwaani katika vazi la ufukweni.
PICHA ZOTE ZA http://mrokim.blogspot.com/2012/11/show-ya-redds-miss-tanzania-2012-ndo.html
PICHA ZOTE ZA http://mrokim.blogspot.com/2012/11/show-ya-redds-miss-tanzania-2012-ndo.html
Comments