Monday, November 05, 2012

UJUMBE WA BODI YA UTALII TANZANIA (TTB) WATEMBELEA KLABU YA SUNDRLAND FC

 
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akizungumza na Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband wakati ujumbe wa TTB ulipotembelea Uwanja wa Sunderland FC na kushuhudia mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya timu hiyo na timu ya Aston Villa uliofanyika siku ya jumamosi nchini Uingereza, Bodi ya utalii Tanzania inatangaza matangazo ya utalii wa Tanzania katika viwanja sita vinavyotumika kuchezea ligi kuu ya Uingereza (Premier Liegue) kikiwemo kiwanja cha Sunderland FC, katika picha katikati ni Edmund Hazal Mkurugenzi wa Kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo hayo,Bw. David Miliband pia ni mwenyekti wa klabu ya Sunderland.   
Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband  akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena kushoto mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya Suderland na Aston Villa, David Miliband pia ni mwenyekiti wa klabu ya Suderland
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya UtaliiTanzania TTB Devotha Mdachi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani na maafisa wa timu ya Sunderland FC baada ya kukabidhiwa zawadi ya saa kutoka kulia ni Balozi wa Sunderland na Golikipa wa zamani Jimmy Montgomery, Gary Mutchinson Mkurugenzi wa Biashara na Kevin Ball Nahodha wa zamani wa timu hiyo.
 
Balozi wa Sunderland na Golikipa wa zamani Jimmy Montgomery kiutambulisha ujumbe wmaafisa wa bodi ya utalii TTB ulipotembelea uwanja huo.
 
Ujumbe wa bodi ya Utalii Tanzania ukishuhudia mchezo huo.
 
Ujumbe wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB akipiga picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Sunderland katika hafla hiyo wa pili kutoka kulia waliosimama nyuma ni James MacFadden wa nne ni David Meyler na wa sita ni Titus Brambie.
 
Hapa ndiyo lango kuu la kuingilia kwenye jukwaa kuu la uwanja huo
 
Ujumbe wa Bodi ya Utalii na maafisa wa taasisi mbalimbali wakipiga picha ya pamoja nje ya uwanja huo kutoka kulia ni Bw. Manase kutoka Ngorongoro, Bw. Mukhtar kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki , Mkurugenzi wa Masoko TTB Devotha Mdachi, Geofrey Meena Meneja Masoko TTB na Edmond Hazal Mkurugenzi wa kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo hayo katika viwanja vya ligi kuu Uingereza.nin

No comments: