Thursday, November 08, 2012

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI DHIDI YA RUFAA YA LEMA

IMG-20121108-WA0003
Kutoka kushoto, Henry Kileo, Nuru Ndosi na Mhe. Godbless Lema wakiwa mahakamani leo.
IMG-20121108-WA0007
Godbless Lema akiwasili katika viwanja vya Mahakama ya Kuu jijini Dar leo.
Pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufani kupitia Wakili wao Alute Mughwai  ili rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa ubunge isisikilizwe limetupiliwa mbali na Mahakama baada ya kuridhika kwamba kosoro zilizolalamikiwa zilikuwa kwa upande wa Mahakama.
Pia kifungu kilichomhukumu Lema kina makosa hivyo kesi itatajwa tena baada ya siku 14 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza hoja za waliokata rufaa.
Mawakili wa Mhe. Godbless Lema wanahitajika kutimiza mahitaji fulani ya kisheria ndani ya siku 14 ili shauri la rufaa hiyo iweze kupangiwa siku ya kusikilizwa na kuamuliwa.
Wadaiwa kwenye shauri hilo ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.
Lema anawakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu.

No comments: