("fastjet" au Kampuni”)
Mauzo ya tiketi
za fastjet yazinduliwa Tanzania
Nauli za chini
zaidi kuwahi kutokea kuna maana Watanzania wengi zaidi wanaweza kupaa
13 Novemba 2012, Dar es Salaam - fastjet, Shirika la ndege la kwanza
Afrika la nauli nafuu, leo limezindua mauzo ya tiketi zake nchini Tanzania,
ikiwa ni maandalizi ya safari yake ya kwanza ya kibiashara mwishoni
mwa mwezi huu.
Uzinduzi huo wa tiketi ni hatua muhimu katika juhudi za kampuni kuwezesha
usafiri wa ndege kwa Watanzania wako wengi ambao awali walikuwa hawamudu
gharama za safari za ndege. Huku nauli za anga zikiwa zinaanzia Tsh32,
000 (U$D20) kabla ya kodi za serikali, usafiri wa anga sasa unakuwa
moja ya njia nafuu za watu kusafiri.
fastjet, ambayo imeinunua Fly540, imechagua Dar es Salaam kuwa kituo
chake cha kwanza cha uendeshaji barani Afrika, huku safari za ndege
zikiwa zimepangwa kuanza kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere kuanzia Novemba 29. Tiketi za Dar es Salaam – Kilimanjaro
na Dar es Salaam – Mwanza zinaanza kuuzwa kuanzia leo. Safari zingine,
za ndani na kanda ya Mashariki mwa Afrika, zitaanza baada ya wiki kadhaa.
Akizungumzia uzinduzi wa mauzo ya tiketi, Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet,
Ed Winters alisema:
“Hiki ni kipindi cha kihistoria kwa safari za anga Tanzania, na
hasa Afrika. Usafiri wa anga siyo tena himaya ya watu wachache Tanzania.
fasyjet itafanya usafiri wa anga kuwa kitu ambacho Watanzania wengi
wanakimudu tofauti na awali, na hivyo kutoa fursa nzuri zaidi kwa biashara,
safari za likizo, na wanafamilia kutembeleana. Tunawashukuru wabia wetu
Tanzania kwa ushirikiano wao mpaka leo hii, na tunamatumaini ya uhusiano
mrefu na wenye manufaa kwa watanzania.”
Tiketi zinapatikana kupitia mawakala wa usafiri na dawati la mauzo,
kituo cha mawasiliano na ofisi za fastjet yenyewe. Tovuti mpya ya fastjet,
www.fastjet,com itazinduliwa wiki ijayo na kutoa taarifa za safari na
nauli. Tovuti hiyo pia itaruhusu kununua tiketi kwa kutumia kadi za
credit/debit pamoja na simu za mkononi.
Uzinduzi wa
Chapa ya fastjet
Fastjet pia imezindua chapa yake mpya kabla ya kuanza kwa safari zake
za kibiashara. Nembo ya kampuni ni kasuku (kasuku wa kijivu wa
Afrika) ambaye alichaguliwa kutokana na sifa zake za maarifa, urafiki
na kuakisi kaulimbiu ya fastjet ambayo ni usafiri wa akili. Wiki hii
pia itashuhudia uzinduzi wa mtandao wa kijamii wa fsaftjet kupitia Facebook
na Twitter na hivyo kutoa ukumbi kwa wateja na wadau Kuwasiliana na
kuchangia mawazo yao kuhusu kampuni kwa njia ya mtandao.
Richard Bodin, Afisa Biashara Mkuu wa fastjet anasema:
“Moja ya hulka kuu za fastjet ni uwazi. Tunataka kuziba pengo kati
ya mlaji na shirika la ndege kwa kuhakikisha tunakuwa na mawasiliano
ya pamoja kila inapowezekana na kusikiliza mahitaji na vipaumbele vya
wateja. Mitandao ya kijamii ni njia bora ya kufanikisha hili – kumbi
kama Facebook na Twitter hutuwezesha kuwasiliana moja kwa moja na wateja
na kutusaidia sisi kuelewa vizuri zaidi na kuiwezesha fastjet kwenda
sambamba na mahitaji na mapendeleo ya wadau wetu.
Shirika lina ndege tatu za kisasa aina ya Airbus A319. Ndege zote
tatu zimo kwenye mchakato wa kupakwa rangi na nembo za fastjet kabla
ya kuletwa Tanzania tayari kwa uzinduzi wa safari za kibiashara baadae
mwezi huu.
MWISHO
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:
africapractice Tanzania Tel: +255 (0)222 668 389
Teweli Teweli
Meg Muigai
Citigate Dewe Rogerson, London Tel:+44 (0) 20 7638 9571
Angharad Couch
Eleni Menikou
TAARIFA KWA
WAHARIRI
Kuhusu fastjet Plc
fastjet Plc ni kampuni mama ya Shirika la Ndege la Afrika Fly540,
ambalo hujiendesha kutoka vituo vinne Kenya, Tanzania, Ghana na Angola.
Kwa sasa Fly540 ina ndege 10 zenye kuhudumia kama njia 25 za ndani na
kanda, ikibeba takriban abiria 750,000 kwa mwaka, huku ikiwa na msisitizo
mkubwa kwenye usalama, ulinzi na kuaminika.
Baada ya mashauriano na mwanzilishi wa easyjet, Sir Stelios Haji-Ioannou,
kampuni ya easyGroup ililenga kubaini uwezekano wa kuwa na shirika la
ndege la nauli nafuu Afrika, kama ilivyo Ulaya, na hivi sasa tunajiandaa
kuzindua fastjet, shirika la kwanza la ndege Afrika la nauli nafuu,
likiwa na ndege za kisasa kwa kutumia leseni na njia za Fly540. Safari
za kwanza kwa kutumia chapa ya fastjet zinatarajiwa kuanza mwishoni
mwa Novemba, na hivyo kuja na aina mpya kabisa ya safari za anga kwenye
soko la Afrika.
fastjet Plc imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la London (LSE). Kwa
maelezo zaidi, tembelea www.fastjet.com
Comments