Tuesday, November 13, 2012

KIKWETE AJIUZULU UENYEKITI WA CCM; ATARAJI KUCHAGULIWA TENA KWA KISHINDO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho kupisha uchaguzi kufanyika upya.
Licha ya kujiuzulu lakini Rais Kikwete anataraji kuchaguliwa tena kwa kishindo kwani ndiye mgombea pekee wa nafasi hiyo ya Uenyekiti.
Kufuatia kujiuzulu huko nafasi ya Uenyekiti imeshikiliwa kwa muda na Rais Mstaafu, Benjamini William Mkapa aliyeungwa mkono na wajumbe wote baada ya jina lake kupendekezwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake.
Mbali na Mywenyerkiti pia Sekretarieti yote ya chama hicho imejiuzulu na inasubiri kuchaguliwa tena baada ya uchaguzi kukamilika.
 Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Salim Asas Abri akiwa na viongozi wa UVCCM Iringa.
Wajumbe wa CCM kutoka mkoa wa Arusha wakiongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa wakifuatilia matukio ya kampeni ndani ya ukumbi wa Kizota wakati kampeni za wagombea nafasi ya Uenyekiti na Makamu Mwenyekiti bara na visiwani zikiendelea.
 Wajumbe wa Mkoa wa Iringa wakjifuatilia kwa umakini kampebni hizo, ambazo zilikuwa zikifanywa na Yusufu Makamba na Vuai Vuai kwaajili ya mgombea wa Uenyekiti.
 Nchimbi akiwa na wajumbe wenzake mkutanoni hapo.
 Wajumbe wa CCM kutoka mkoa wa Arusha  wakifuatilia matukio ya kampeni ndani ya ukumbi wa Kizota wakati kampeni za wagombea nafasi ya Uenyekiti na Makamu Mwenyekiti bara na visiwani zikiendelea.
 Wanachama wa CCM, kundi la Diaspora wakipiga picha na Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM Taifa.
 Wanachama wa CCM, kundi la Vyuo Vikuu wakipiga picha na Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM Taifa.
  Vijana wa Chuo kikuu ambao ni makada wa CCM wakiwa pamoja
 Wajumbe kutoka Mwanza wakimsikiliza Mzee Yusuf Makamba akimnadi Jakaya Kikwete.
 Wajumbe kutoka Kagera wakifuatilia kampeni. Picha zote kwa hisani ya FATHER KIDEVU

No comments: