Rais Jakaya Kikwete Ashiriki Mazishi ya Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mhashamu Baba Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga baada ya kuwasili kwenye Kanisa la Mama wa Huruma katika Parokia ya Ngokolo mjini Shinyanga kushiriki mazishi ya Askofu huyo jana, Jumamosi, Novemba 10, 2012.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mhashamu Baba Askofu Aloysious Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga wakati wa mazishi wa Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga jana.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Askofu Aloysius Balina wakati wa mazishi ya Askofu huyo jana kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, mjini Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga wakati wa mazishi ya Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, Shinyanga jana. Picha na mdau Fred Maro-Ikulu

Comments