SIMBA MAJANGA!!! WACHAPWA NA TOTO 1-0 TAIFA

 
BAO pekee la Mussa Said Kimbu dakika ya 73, leo limeizamisha Simba SC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 
Kimbu alifunga bao hilo akiunganisha krosi ya Mganda, Mohamed Jingo tena akipitisha mpira katikati ya msitu wa mabeki wa Simba na kipa wao, Wilbert Mweta.
 
Simba hawakucheza vizuri kama timu leo, ila kwa mchezaji mmoja mmoja, karibu kila mchezaji alicheza vizuri na Emanuel Okwi ndiye aliyekuwa akiisumbua zaidi ngome ya Toto.
 
Katika michezo mingine ya ligi hiyo, Azam imefungwa 2-1 na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
 
Kwa matokeo hayo, Yanga inazidi kujinafasi kileleni kwa pointi zake 26, baada ya kucheza mechi 12 na kesho itahitimisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kwa kucheza Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
 
Simba inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 23 na Azam yenye pointi 24 ni ya pili.
Simba SC: Wilbet Mweta, Nassor Masoud ‘Chollo’, Paul Ngalema, Komanbil Keita, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto/Edward Christopher, Mrisho Ngassa/Haruna Chanongo, Felix Sunzu na Emanuel Okwi.   
 
Toto; Erick Ngwengwe, Ally Ahmad, Eric Murilo/Robert Magadula, Evarist Maganga, Peter Mutabuzi, Hamisi Msafiri, Emanuel Swita/James Magafu, Kheri Mohamed/Mohamed Hussein, Mohamed Jingo, Suleiman Kibuta na Mussa Said.  SOURCE: BIN ZUBERY BLOG

Comments