
Head of Commonwealth, Queen Elizabeth II take a group photo with the commonwealth Head of Government soon after she opening the meeting. Photo/ State House

Head of Commonwealth, Queen Elizabeth II take a group photo with the commonwealth Head of Government soon after she opening the meeting. Photo/ State House.
British Queen Elizabeth II (R) and President of Uganda Yoweri Kaguta Museveni (L) attend the opening ceremony of the 2007 Commomwealth Heads of Government Meeting (CHOGM) in Kampala, Uganda, Nov. 23, 2007. Delegates from 53 Commomwealth member states are present at the 3-day meeting. (Xinhua/Wang Ying)

Commonwealth Secretary-General Don McKinnon (standing) speaks during the opening ceremony of the 2007 Commomwealth Heads of Government Meeting (CHOGM) in Kampala, Uganda, Nov. 23, 2007. Delegates from 53 Commomwealth member states are present at the 3-day meeting Photo by Xinhua.
Wakuu wa nchi 53 waanza mkutano Kampala
KAMPALA, Uganda
MKUTANO wa Viongozi wa nchi za Jumuia ya Madola (Chogm) umeanza rasmi jana mjini Kampala,k ikihudhuriwa na Malkia Alizabeth II wa Uingereza na mumewe Duke wa Edinburg.
Mkutano huo wa siku tatu unaowakutanisha viongozi 53 wa nchi wanachama wa jumuia hiyo ulifunguliwa rasmi jana na Malkia Eizabeth II kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena mjini Kampala.
Taairfa zinasema kuwa hata hivyo mkutano huo ambao kwa mujibu wa ratiba ulitakiwa kufunguliwa rasmi saa 3.00 asubuhi ulichelewa kuanza kwa takribani saaa nzima.
Malkia wa Uingereza Nni mkuu wa moja wka moja wa Jumuia hiyo hasa kutokna na wadhifa wake, alifika nchini Uganda juzi, pamoja na mambo mengine alweza kuhutubia Bunge la nchi hiyo.
Ni utaratibu uliozoeleka kwa Malkia kutembelea nchi mwenyeji wa mkutano huo unaowakutanisha viongozi wa nchi 53 nyingi zikiwa ni zile zilizowahi kuwa makoloni ya Uingereza kila unapofanyika mara moja kila baada ya miaka miwili.
Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo Don McKinon alisema pamoja na uamuzi uliotolewa jana asubuhi juu ya Pakistan, mkutano huo unatarajiwa kutoka na majibu juu ya namna ya kuimarisha Demokrasia, Biashara ya Kimataifa, Malengo ya Milenia yanayotakiwa kufikiwa mwaka 2015 na kupata taaarifa ya uitendaji kwenye makubaliano walioyofikia katika mkutano uliopita uliofanyika mwa 2005 Visiwa vya Malta.
Pia viongozi haoo watajadili suala la Uanachama wa nchi rafiki na jirani wa Uganda, Rwanda baada ya maombi yaliyofikishwa ikiomba kuwa mwanachama, huku Rais Kagame akiwa ni miongoni mwa viongozi walioshiriki hatua za awali za maandalizi ya mkutano huo wa wakuu wa nchi.
Hata hivyo taarifa za awali zinasema pamoja na uwezekano uliopo. Suala hilo ltaweza kuthibitishwa rasmi kwenye mkutano wa mwaka 2009, baada ya suala hilo kujadiliwa kwenye mkutano huu na kufikia uamuzi.
Pia katika mktano ao huo, viongozi hao watamchagua Katibu Mkuu mpya wa Jumuia hiyo atakayemrithi Don McKinon ambaye anamaliza muda wake Machi mwaka kesho. Miongoni mwa wanaowania naffasi hiyo ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Malta Michael Frendo, Mwakilishi wa India nchini Uingereza Kamalesh Sharma na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Jumuia hiyo Mohan Kaul.