Friday, October 10, 2008

Johannesburg ya Tanzania


Inaitwa Johannesburg Hotel ni hoteli matata sana hapa jijini Dar, viwango vyake ndugu yangu bila shaka vinaonekana kwa macho ya kawaida, ipo katika maeneo poa sana. Picha kwa hisani ya mdau wa charaz.blogspot.com

Thursday, October 09, 2008

Daraja la Mto Ruvu Juu: Kiungo Muhimu cha Usafiri na Maendeleo

Daraja la Mto Ruvu Juu ni mojawapo ya miradi mikubwa ya miundombinu inayotekelezwa nchini Tanzania kwa lengo la kuboresha usafiri na kukuza uchumi. Daraja hili, ambalo ujenzi wake uko katika hatua za mwisho, linapita juu ya Mto Ruvu, mojawapo ya mito mikubwa inayopeleka maji Bahari ya Hindi.

Umuhimu wa Daraja la Mto Ruvu Juu

Daraja hili ni sehemu ya barabara kuu inayounganisha Dar es Salaam na mikoa ya Kaskazini na Magharibi mwa Tanzania. Kukamilika kwake kutapunguza msongamano wa magari, kuboresha usafirishaji wa bidhaa, na kurahisisha safari za abiria wanaotumia njia hii kila siku.

Sifa za Kijenzi

  • Muundo Imara: Daraja limejengwa kwa teknolojia ya kisasa ili kuhimili uzito mkubwa wa magari na mabadiliko ya hali ya hewa.
  • Urefu na Upana: Limepanuliwa ili kupunguza msongamano, likiwa na njia zaidi za magari na sehemu za waenda kwa miguu.
  • Ustahimilivu: Umeimarishwa kwa zege na vyuma vyenye viwango vya juu vya uimara ili kudumu kwa muda mrefu.

Manufaa kwa Jamii na Uchumi

  • Kupunguza Foleni: Daraja jipya litapunguza muda wa kusafiri kati ya Dar es Salaam na mikoa mingine.
  • Kukuza Biashara: Usafirishaji wa mazao, bidhaa, na huduma utakuwa rahisi na wa haraka zaidi.
  • Kuongeza Usalama: Ujenzi wa daraja hili umezingatia viwango vya kisasa vya usalama wa barabara.

Mwonekano na Mandhari

Abiria wanaopita eneo la Ruvu wanapata fursa ya kuona mandhari nzuri ya mto huu, ukiwa umezungukwa na uoto wa asili na mashamba ya mazao. Daraja hili linatarajiwa kuwa kivutio kingine cha kipekee kwa wapenda safari na wapiga picha.

Kwa ujumla, Daraja la Mto Ruvu Juu ni mradi wa kimkakati unaotarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafiri na uchumi wa Tanzania. Kukamilika kwake kutakuwa hatua kubwa katika juhudi za serikali kuboresha miundombinu ya nchi.

kampeni


Pichani ni moja ya mabango ya vijana wa CHADEMA kumlalamikia kamanda wa kikosi maalum Venance Tossi kutokana na kusambaratishwa jumatatu usiku baada ya kutuhumiwa kufanya maandamano bila ya kibali.


pichani ni moja ya mabango ya vijana wa CHADEMA kumlalamikia kamanda wa kikosi maalum Venance Tossi kutokana na kusambaratishwa jumatatu usiku baada ya kutuhumiwa kufanya maandamano bila ya kibali. picha zote na Mussa Juma.

Tuesday, October 07, 2008

Mbowe mzima


mwenyekiti wa CHADEMA, Freman Mbowe akizungumza katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Menonite jana mara baada ya kuwasili Tarime kutoka Jijini Dar es Salaam ambapo alipokewa na maandamano makubwa kutokea mpakani mwa wilaya ya Tarime na Rolya zaidi ya kilometa 25 toka Tarime mjini. Picha na Mussa Juma

Happy Birthday Mheshimiwa Rais

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo (Jumanne, Oktoba 7, 2008) ameadhimisha Siku yake ya kuzaliwa kwa kuhudhuria hafla fupi ya kushtukiziwa aliyoandaliwa na wafanyakazi wenzake wa Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Kikwete amefikisha umri wa miaka 58 leo. Alizaliwa Oktoba 7, 1950 katika kijiji cha Msoga, Chalinze, Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Katika halfa hiyo kwenye makazi yake rasmi, Rais Kikwete amepata nafasi ya kumsalimia binafsi kila mmoja wa wafanyakazi hao baada ya kuwa ameshiriki nao katika kuonja keki ya Siku hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi hao katika halfa hiyo fupi, Katibu Mkuu wa Ikulu, Michael Mwanda amempongeza Rais Kikwete kwa kufikisha umri wa miaka 58 na kumtakia afya njema na maisha marefu.

Naye Rais amewashukuru wafanyakazi hao akisema kuwa utawala wake usingepata mafanikio yaliyopatikana bila kazi kubwa inayofanywa na wafanyakazi hao.

“Nawashukuruni sana kwa kunisaidia kwa kiasi kikubwa. Nawashukuruni pia kwa kuniandalia hafla hii fupi ya kushtukizia kwa sababu kama unavyojua sisi watu tuliozaliwa vijijini hatuna utamaduni wa namna hii wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa ama kulishana keki.”

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

07 Oktoba, 2008

Monday, October 06, 2008

ajali Tarime


Picha ya kwanza ni baadhi ya polisi pamoja na Wagombea wa ubunge jimbo la Tarime, Christopher Nangoye (CCM) mwenye shati na kijani na Charles Mwera anayemfuata wakibeba miili ya watu waliofariki katika ajali ya gari jana baada ya gari walilokuwa wamepanda kuangukiwa na Lori katika eneo la Mikoa jirani na Tarime. Watu watano walifariki katika ajali hiyo.

Rais Ravalomanana awasili


Makamau wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Madagaska Bw. Marcravalomanana, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kiserikali.

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...